Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Zin
Hesabu 13 : 21
21 Basi wakapanda wakaipeleleza nchi toka jangwa la Sini hadi Rehobu, mpaka kuingia Hamathi.
Hesabu 20 : 1
1 ⑯ Kisha wana wa Israeli, mkutano wote, wakaingia jangwa la Sinai, katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadeshi; Miriamu akafa huko, akazikwa huko.
Hesabu 27 : 14
14 kwa sababu mliasi juu ya neno langu katika jangwa la Sini wakati wa mateto ya mkutano, wala hamkunistahi, hapo majini, mbele ya macho yao. (Maji hayo ndiyo maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.)
Hesabu 33 : 36
36 Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapiga kambi katika nyika ya Sini (ni Kadeshi).
Hesabu 34 : 4
4 ⑯ kisha mpaka wenu utageuka kwenda upande wa kusini wa kukwelea kwake Akrabimu, kisha kupita kwendelea Sini; na kutokea kwake kutakuwa kuelekea upande wa kusini wa Kadesh-barnea; kisha utaendelea mpaka Hasar-adari, na kufikia Azmoni;
Kumbukumbu la Torati 32 : 51
51 ⑪ kwa sababu mlinikosa ninyi juu yangu katikati ya wana wa Israeli katika maji ya Meriba huko Kadeshi, katika bara ya Sini; kwa kuwa hamkunitakasa katikati ya wana wa Israeli.
Yoshua 15 : 1
1 Sehemu waliyopewa wana wa Yuda kwa kufuata jamaa zao ilikuwa imefika mpaka wa Edomu, hadi jangwa la Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini.
Yoshua 15 : 3
3 nao ukaendelea upande wa kusini wa kukwea kwenda Akrabimu, kisha ukaendelea hadi Sini, kisha ukaenda upande wa kusini wa Kadesh-barnea, kisha ukaendelea karibu na Hesroni, kisha ukafika Adari, na kuzunguka kwendea Karka;
Leave a Reply