Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Zabuloni
Mwanzo 30 : 20
20 Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni.
Mwanzo 35 : 23
23 Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
Mwanzo 46 : 14
14 Na wana wa Zabuloni; Seredi, na Eloni, na Yaleeli.
Mwanzo 49 : 13
13 Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
Kutoka 1 : 3
3 na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini;
1 Mambo ya Nyakati 2 : 1
1 ② Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;
Mwanzo 46 : 14
14 Na wana wa Zabuloni; Seredi, na Eloni, na Yaleeli.
Hesabu 26 : 27
27 Hawa ndio jamaa wa Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na mia tano.
Hesabu 2 : 3
3 Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa bendera ya kambi ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.
Hesabu 2 : 7
7 ① na kabila la Zabuloni; na mkuu wa wana wa Zabuloni atakuwa Eliabu mwana wa Heloni;
Hesabu 10 : 14
14 Mahali pa mbele ilisafiri beramu ya kambi ya wana wa Yuda, kwa majeshi yao; na Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyekuwa juu ya jeshi lake.
Hesabu 10 : 16
16 Na juu ya jeshi la kabila la wana wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni.
Mwanzo 49 : 13
13 Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
Yoshua 19 : 16
16 ⑦ Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
Mathayo 4 : 13
13 akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;
Waamuzi 1 : 30
30 Zabuloni naye hakuwatoa wenyeji wa Kitroni, wala hao waliokaa katika Nahalali; lakini Wakanaani walikaa kati yao, wakalazimishwa shokoa.
Yoshua 21 : 35
35 na Dimna pamoja na mbuga zake za malisho, na Nahalali pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne.
1 Mambo ya Nyakati 6 : 77
77 Nao mabaki ya Walawi, wana wa Merari, wakapewa, katika kabila la Zabuloni; Rimona pamoja na viunga vyake, na Tabori pamoja na viunga vyake;
Kumbukumbu la Torati 33 : 19
19 Watayaita mataifa waje mlimani; Wakasongeze huko sadaka za haki; Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari, Na akiba zilizofichamana za mchangani.
Leave a Reply