Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yordani
Yoshua 15 : 5
5 Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hadi mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;
Mwanzo 32 : 10
10 ⑧ mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.
Yoshua 2 : 7
7 Basi hao watu wakawafuata kwa njia iendayo Yordani mpaka vivukoni; na mara wale watu waliowafuatia walipokwisha kutoka, wakalifunga lango.
Waamuzi 3 : 28
28 Akawaambia, Nifuateni; kwa kuwa BWANA amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakateremka na kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha mtu kuvuka.
Waamuzi 7 : 24
24 ⑯ Kisha Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima vilima ya Efraimu, akisema, Haya, teremkeni juu ya Midiani, na kuyatwaa hayo maji mbele yao, mpaka Bethbara, maana huo mto wa Yordani. Basi wanaume wote wa Efraimu walitokeza wakayatwaa maji mpaka Bethbara, yaani, huo mto wa Yordani.
Waamuzi 8 : 4
4 Basi Gideoni akafika Yordani, akauvuka, yeye na hao watu mia tatu waliokuwa pamoja naye, walikuwa wamechoka, lakini waliendelea kuwafuatilia adui.
Waamuzi 10 : 9
9 Wana wa Amoni nao wakavuka Yordani ili wapigane na Yuda, na kupigana na Benyamini, na nyumba ya Efraimu; basi hivyo Israeli walikuwa wanasumbuliwa sana.
Waamuzi 12 : 6
6 ndipo walipomwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka watu elfu arubaini na mbili wa Efraimu wakati huo.
2 Samweli 2 : 29
29 ⑦ Wakaenda Abneri na watu wake usiku ule wote kati ya ile Araba; wakavuka Yordani, wakapita kati ya Bithroni yote, wakaja Mahanaimu.
2 Samweli 17 : 22
22 Ndipo Daudi, na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaondoka, wakavuka Yordani; na kulipopambazuka hakubaki hata mmoja wao asiyevuka Yordani.
2 Samweli 17 : 24
24 ⑫ Basi Daudi akaja Mahanaimu. Naye Absalomu akauvuka Yordani yeye na watu wote wa Israeli pamoja naye.
2 Samweli 19 : 15
15 Hivyo mfalme akarudi, akafika Yordani. Kisha watu wa Yuda wakaja Gilgali kumlaki mfalme, na kumvusha mfalme Yordani.
2 Samweli 19 : 31
31 ② Tena Barzilai, Mgileadi, akashuka kutoka Rogelimu; akavuka Yordani pamoja na mfalme, amvushe Yordani.
1 Mambo ya Nyakati 19 : 17
17 Alipoambiwa Daudi; akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akawajia, akapanga vita juu yao. Basi Daudi alipopanga vita juu ya Washami, wakapigana naye.
Yoshua 3 : 15
15 ⑯ basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno),
Yeremia 12 : 5
5 ⑥ Ikiwa umepiga mbio pamoja na hao waendao kwa miguu, nao wamekuchosha, basi wawezaje kushindana na farasi? Na ujapokuwa katika nchi ya amani uko salama, lakini utafanyaje hapo katika kiburi cha Yordani?
1 Mambo ya Nyakati 12 : 15
15 Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.
Yoshua 5 : 1
1 Ikawa, wafalme wa Waamori, waliokaa ng’ambo ya Yordani pande za magharibi, na wafalme wote wa Wakanaani, waliokuwa karibu na bahari, waliposikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya Yordani mbele ya wana wa Israeli, hadi tulipokwisha kuvuka, basi mioyo yao iliyeyuka, wala haikuwamo roho ya nguvu ndani yao tena; kwa ajili ya wana wa Israeli.
Zaburi 114 : 3
3 Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma.
Leave a Reply