Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yoabu
1 Mambo ya Nyakati 2 : 16
16 ⑬ na dada zao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.
2 Samweli 8 : 16
16 ⑥ Huyo Yoabu, mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa majeshi; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, mwekaji kumbukumbu;[8]
2 Samweli 20 : 23
23 Basi Yoabu alikuwa akiongoza jeshi lote la Israeli; na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa akiwaongoza Wakerethi, na Wapelethi;
1 Mambo ya Nyakati 11 : 6
6 Naye Daudi akasema, Mtu yeyote atakayekuwa wa kwanza wa kuwapiga Wayebusi, yeye atakuwa mkuu na jemadari. Naye wa kwanza aliyepanda ni Yoabu mwana wa Seruya, naye akawa mkuu.
1 Mambo ya Nyakati 18 : 15
15 Na Yoabu mwana wa Seruya akawa mkuu wa jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe.[12]
1 Mambo ya Nyakati 27 : 34
34 na, baada ya Ahithofeli, walikuwa Yehoyada mwana wa Benaya, na Abiathari; na jemadari wa jeshi la mfalme alikuwa Yoabu.
1 Mambo ya Nyakati 26 : 28
28 Na vyote alivyoviweka wakfu Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, na Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya; na mtu yeyote aliyekiweka wakfu kitu chochote, kilikuwa chini ya mkono wa Shelomothi na nduguze.
1 Mambo ya Nyakati 11 : 6
6 Naye Daudi akasema, Mtu yeyote atakayekuwa wa kwanza wa kuwapiga Wayebusi, yeye atakuwa mkuu na jemadari. Naye wa kwanza aliyepanda ni Yoabu mwana wa Seruya, naye akawa mkuu.
2 Samweli 2 : 32
32 ⑧ Nao wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake, lililokuwako Bethlehemu. Yoabu na watu wake wakaenda usiku kucha, wakapambazukiwa huko Hebroni.
2 Samweli 3 : 27
27 Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hadi katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hadi akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.
1 Wafalme 2 : 5
5 ⑥ Na zaidi ya hayo, unajua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kumwaga damu wakati wa amani akilipiza kisasi cha vita, mshipi akautia damu ya vita uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.
1 Wafalme 11 : 16
16 (kwa kuwa Yoabu alikaa huko miezi sita pamoja na Israeli wote, hadi alipompoteza kila mwanamume wa Edomu);
Zaburi 60 : 1
1 Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena.
2 Samweli 10 : 14
14 Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akarudi kutoka kwa wana wa Amoni, akaja Yerusalemu.
1 Mambo ya Nyakati 19 : 15
15 Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, nduguye, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akaja Yerusalemu.
2 Samweli 11 : 1
1 Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza Waamoni, wakauzingira Raba. Lakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu.
2 Samweli 11 : 25
25 Basi Daudi akamwambia yule mjumbe, Basi, mwambie Yoabu maneno haya, Jambo hili lisiwe baya machoni pako, maana upanga hula huyu kama unavyomla huyu; zidi kutia nguvu vita vyako juu ya mji ukauangushe; nawe mtie moyo.
2 Samweli 12 : 29
29 Basi Daudi akawakusanya watu wote akaenda Raba, akapigana nao, akautwaa.
1 Mambo ya Nyakati 20 : 1 – 104
1 Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauzingira Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza.
2 Kisha Daudi akatwaa taji la Milkomu[13] toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.
3 Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawawafanyisha kazi kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.
4 Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai;[14] nao Wafilisti[15] wakashindwa.
5 Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi,[16] Mgiti, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.
6 Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai.[17]
7 Naye huyo alipowatukana Israeli, Yonathani, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua.
8 Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai[18] wa Gathi, nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mkono wa watumishi wake.
Leave a Reply