Biblia inasema nini kuhusu Wema – Mistari yote ya Biblia kuhusu Wema

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wema

Mambo ya Walawi 19 : 34
34 Mgeni aishiye pamoja nawe atakuwa kama mzaliwa kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Kumbukumbu la Torati 22 : 4
4 Umwonapo punda wa nduguyo, au ng’ombe wake, ameanguka kando ya njia, usijifiche kama usiyemwona; sharti umsaidie kumwinua tena.

Zaburi 112 : 5
5 ⑱ Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki.

Mithali 14 : 21
21 Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri.

Mithali 19 : 22
22 Haja ya mwanadamu ni hisani yake; Ni afadhali maskini kuliko mwongo.

Mithali 31 : 26
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake.

Isaya 11 : 13
13 Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu.

Zekaria 7 : 10
10 tena msimdhulumu mjane, wala yatima, wala mgeni, wala maskini; wala mtu awaye yote miongoni mwenu asiwaze mabaya juu ya ndugu yake moyoni mwake.

Mathayo 5 : 7
7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

Mathayo 5 : 42
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Luka 6 : 30
30 Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.

Mathayo 25 : 36
36 nilikuwa uchi, mkanivika nilikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nilikuwa kifungoni, mkanijia.

Luka 6 : 35
35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.

Matendo 20 : 35
35 Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.

Warumi 12 : 15
15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.

Warumi 15 : 2
2 Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe.

Warumi 15 : 5
5 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunuia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa kufuata mfano wa Kristo Yesu;

1 Wakorintho 13 : 7
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

Wagalatia 6 : 2
2 Mchukuliane mizigo na hivyo kuitimiza sheria ya Kristo.

Wagalatia 6 : 10
10 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.

Waefeso 4 : 32
32 ⑱ tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Wakolosai 3 : 12
12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

Wakolosai 3 : 14
14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

1 Timotheo 5 : 10
10 na awe ameshuhudiwa kwa matendo mema; katika kulea watoto, kuwa mkaribishaji, kuwaosha watakatifu miguu, kuwasaidia wateswao, na kujitolea kutenda wema katika hali zote.

Waraka kwa Waebrania 5 : 2
2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe ana udhaifu;

1 Petro 3 : 9
9 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.

1 Petro 4 : 8
8 Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.

2 Petro 1 : 7
7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *