wanyama

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia wanyama

Mathayo 6 : 26
26 ⑥ Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?

Mithali 12 : 10
10 Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili.

Mhubiri 3 : 18 – 21
18 Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.
19 ⑲ Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.
20 ⑳ Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.
21 Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?

Mwanzo 1 : 30
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

Mwanzo 1 : 21
21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Zaburi 145 : 9
9 ⑪ BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake ziko juu ya vyote alivyoumba.[25]

Ayubu 35 : 11
11 Atufundishaye zaidi ya wanyama wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?

Isaya 65 : 25
25 Mbwamwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema BWANA.

Luka 12 : 24
24 ① Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!

Yakobo 3 : 7
7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

Ayubu 12 : 7
7 Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na ndege wa angani, nao watakuambia;

Mwanzo 8 : 20
20 Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.

Isaya 11 : 6
6 Mbwamwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwanasimba na ng’ombe wanono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.

Mithali 6 : 6 – 8
6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7 Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu,
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

Luka 12 : 6
6 Je! Shomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.

Ayubu 38 : 41
41 ⑪ Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?

Mambo ya Walawi 19 : 19
19 Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja.

Zaburi 147 : 9
9 Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao.

Zaburi 50 : 10 – 12
10 Maana kila mnyama-pori ni wangu, Na mifugo juu ya angani elfu.
11 Nawajua ndege wote wa milima, Na wanyama wote wa mashamba ni wangu.
12 Kama ningekuwa na njaa singekuambia, Maana ulimwengu ni wangu, na vyote vilivyomo.

Mhubiri 3 : 21
21 Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *