Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Wafilisti
Mwanzo 10 : 14
14 ⑫ na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 12
12 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.
Yeremia 47 : 4
4 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
Amosi 9 : 7
7 ③ Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema BWANA? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri?
1 Samweli 30 : 16
16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.
Ezekieli 25 : 16
16 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani.
Sefania 2 : 5
5 Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la BWANA liko juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako.
Mwanzo 10 : 14
14 ⑫ na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 12
12 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.
Yeremia 47 : 4
4 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
Amosi 9 : 7
7 ③ Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema BWANA? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri?
Kutoka 13 : 17
17 Ilikuwa hapo Farao alipowaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakabadili nia watu hawa hapo watakapokumbana na vita, na kurudi Misri;
Kutoka 23 : 31
31 ⑫ Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hadi bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.
Kumbukumbu la Torati 2 : 23
23 ⑱ na Waavi waliokuwa wakikaa katika vijiji mpaka Gaza waliangamizwa na Wakaftori waliotoka Kaftori, na hawa wakakaa badala yao.)
Yoshua 13 : 3
3 kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Yoshua 15 : 47
47 ④ Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kuu na pwani yake.
Yoshua 13 : 3
3 kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Waamuzi 3 : 3
3 ⑱ aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi.
Waamuzi 16 : 5
5 ⑩ Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
Waamuzi 16 : 30
30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.
1 Samweli 5 : 8
8 Basi wakatuma watu waende kuwakusanya kwao wakuu wote wa Wafilisti, wakasema, Tulifanyieje sanduku la Mungu wa Israeli? Nao wakajibu, Sanduku la Mungu wa Israeli na lihamishwe liende Gathi. Wakalihamisha sanduku la Mungu wa Israeli.
1 Samweli 5 : 11
11 Kwa hiyo wakatuma watu waende kuwakusanya wakuu wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake, ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini kote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.
1 Samweli 6 : 4
4 ③ Ndipo wakauliza, Na hayo matoleo ya kosa tutakayompelekea, yatakuwa ya namna gani? Na yawe majipu ya dhahabu matano, na panya wa dhahabu watano, sawasawa na idadi ya wakuu wa Wafilisti; kwa kuwa tauni moja ilikuwa juu yenu nyote, na juu ya wakuu wenu.
1 Samweli 6 : 12
12 Na hao ng’ombe wakashika njia moja kwa moja kwenda Beth-shemeshi; wakaiandama njia ya barabara, wakaenda wakilia, lakini hawakugeukia upande wa kulia wala wa kushoto; na wakuu wa Wafilisti wakawafuata hata kuufikia mpaka wa Beth-shemeshi.
1 Samweli 7 : 7
7 Hata Wafilisti waliposikia ya kuwa wana wa Israeli wamekusanyika huko Mispa, wakuu wa Wafilisti walipanda juu ili kupigana na Israeli. Nao wana wa Israeli waliposikia, wakawaogopa Wafilisti.
Leave a Reply