Biblia inasema nini kuhusu wafia dini – Mistari yote ya Biblia kuhusu wafia dini

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia wafia dini

2 Timotheo 3 : 12
12 ⑰ Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

1 Petro 4 : 14 – 16
14 ⑥ Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.
15 Lakini pasiwe na hata mmoja wenu atakayeteseka kwa kuwa mwuaji, mwizi, mhalifu au hata mfitini.
16 ⑦ Lakini ikiwa mtu yeyote miongoni mwenu anateseka kwa sababu ni Mkristo, asione haya, bali amtukuze Mungu maana ana jina hili.

Warumi 8 : 31 – 35
31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?
32 Yeye ambaye hakumhurumia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje pia kutupa chochote kingine pamoja naye?
33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kulia wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?

Wafilipi 4 : 13
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Ufunuo 6 : 9 – 10
9 ⑩ Na alipoufungua mhuri wa tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
10 ⑪ Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mkweli, utakawia hadi lini kuhukumu na kuilipa damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

Ufunuo 17 : 1 – 18
1 ⑯ Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ⑰ ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wameleweshwa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 ⑱ Akanichukua katika Roho hadi jangwani, nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya kukufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 ⑲ Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 ⑳ Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, Babeli MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu sana.
7 Na yule malaika akaniambia, Kwa nini unastaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi.
8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.
9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja itampasa kukaa muda mfupi.
11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye anaenda kwenye uharibifu.
12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.
14 Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
15 Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.
16 Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.
17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.
18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.

Ufunuo 20 : 4
4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa mamlaka ya kutoa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala kuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *