Biblia inasema nini kuhusu Waamaleki – Mistari yote ya Biblia kuhusu Waamaleki

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Waamaleki

Hesabu 13 : 29
29 Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.

Hesabu 14 : 25
25 Basi Mwamaleki na Mkanaani wakaa katika bonde; kesho geukeni, mkaende jangwani kwa njia iendayo Bahari ya Shamu.[25]

1 Samweli 15 : 7
7 ⑫ Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila hadi Shuri, mashariki mwa Misri.

1 Samweli 27 : 8
8 Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, mpaka nchi ya Misri.

Mwanzo 14 : 7
7 ⑱ Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.

Kutoka 17 : 8
8 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.

Kutoka 17 : 13
13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.

1 Samweli 14 : 48
48 ② Naye kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa mikono ya waliowateka nyara.

1 Samweli 15 : 33
33 Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali.

1 Samweli 27 : 9
9 Tena Daudi akaipiga nchi hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na ng’ombe, na punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi.

1 Samweli 30 : 20
20 Naye Daudi akatwaa makundi yote ya kondoo na ng’ombe, ambao waliwatanguliza mbele ya wanyama wale wengine, wakasema, Hao ndio nyara za Daudi.

1 Mambo ya Nyakati 4 : 43
43 Nao wakawaua Waamaleki waliokuwa wamenusurika, wakakaa huko, hata siku hii ya leo.

Hesabu 14 : 45
45 Ndipo Mwamaleki, na Mkanaani waliokaa huko mlimani, wakateremka, wakawapiga na kuwaangusha, hadi wakafika Horma.

Waamuzi 3 : 13
13 Huyo Egloni akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao wakauchukua huo mji wa mitende.

Kumbukumbu la Torati 25 : 19
19 Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kandokando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.

1 Samweli 28 : 18
18 ④ Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya BWANA, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii BWANA amekutendea hili leo.

Kutoka 17 : 14
14 BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.

Kutoka 17 : 16
16 akasema, BWANA ameapa;[22] BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.

Hesabu 24 : 20
20 Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema, Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa; Lakini mwisho wake atapata uharibifu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *