Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Vita
2 Samweli 22 : 35
35 Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu inaupanda upinde wa shaba.
Waamuzi 12 : 6
6 ndipo walipomwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka watu elfu arubaini na mbili wa Efraimu wakati huo.
2 Samweli 2 : 31
31 Ila watumishi wa Daudi walikuwa wamewapiga watu wa Benyamini, na watu wa Abneri, hata wakafa watu mia tatu na sitini.
2 Samweli 3 : 1
1 ⑩ Basi kulikuwa na vita siku nyingi kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi; Daudi akaendelea akasitawi, lakini nyumba ya Sauli ikaendelea kudhoofika.
1 Wafalme 14 : 30
30 ② Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.
1 Wafalme 16 : 21
21 Ndipo watu wa Israeli wakagawanywa sehemu mbili; nusu ya watu wakamfuata Tibni mwana wa Ginathi, ili wamfanye mfalme; nusu wakamfuata Omri.
Isaya 19 : 2
2 Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.
2 Mambo ya Nyakati 11 : 4
4 BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi wakayatii maneno ya BWANA wakarudi wasiende kupigana na Yeroboamu.
Yoshua 22 : 34
34 Basi hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, wakaiita madhabahu hiyo Edi; wakasema, Kwa kuwa ni ushahidi kati yetu ya kwamba yeye BWANA ndiye Mungu.
2 Wafalme 18 : 36
36 Lakini hao watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana amri ya mfalme ilikuwa kwamba, Msimjibu neno.
2 Mambo ya Nyakati 13 : 12
12 ⑮ Na tazama, Mungu yu pamoja nasi atutangulie, na makuhani wake wenye parapanda, ili wapige sauti ya kuanza vita juu yenu. Enyi wana wa Israeli, msipigane na BWANA, Mungu wa baba zenu; kwani hamtafanikiwa.
Hesabu 31 : 17
17 Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mwanamume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mwanamume kwa kulala pamoja naye.
Kumbukumbu la Torati 2 : 34
34 Tukatwaa miji yake yote wakati huo, tukaharibu kabisa kila mji uliokuwa na wanaume, wanawake na watoto; tusimbakize hata mmoja;
Kumbukumbu la Torati 3 : 6
6 Tukaiharibu kabisa, kama tulivyomfanya huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, kwa kuharibu kabisa kila mji uliokuwa na wanaume, wanawake na watoto.
Kumbukumbu la Torati 20 : 18
18 wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya BWANA, Mungu wenu.
Yoshua 6 : 21
21 ⑥ Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume, wanawake, watoto na wazee, na ng’ombe, kondoo na punda, kwa upanga.
Yoshua 6 : 24
24 Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya BWANA.
Yoshua 8 : 25
25 Wote walioanguka siku hiyo wanaume kwa wanawake, walikuwa ni elfu kumi na mbili, yaani, watu wote wa mji wa Ai.
Yoshua 10 : 40
40 ③ Basi Yoshua akaipiga nchi hiyo yote, nchi ya vilima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela, na nchi ya materemko, na wafalme wake wote; hakumwacha aliyesalia hata mmoja; lakini akawaharibu kabisa wote waliokuwa hai, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Yoshua 11 : 23
23 ⑲ Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote BWANA aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa makabila yao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena.
1 Samweli 15 : 9
9 ⑭ Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.
1 Samweli 27 : 11
11 Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.
Leave a Reply