Biblia inasema nini kuhusu vipodozi – Mistari yote ya Biblia kuhusu vipodozi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia vipodozi

Yeremia 4 : 30
30 ⑧ Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.

Mambo ya Walawi 19 : 28
28 Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.

Kumbukumbu la Torati 22 : 5
5 ⑰ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.

Hosea 2 : 2
2 Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na aondokane na usherati wake usiwe mbele ya uso wake, na uzinzi wake usiwe kati ya matiti yake;

2 Wafalme 9 : 30
30 Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *