Uzushi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uzushi

Tito 3 : 11
11 ⑥ maana unajua ya kuwa mtu kama huyo ni mpotovu na mtenda dhambi, naye amejihukumia hatia yeye mwenyewe.

2 Yohana 1 : 11
11 Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.

Matendo 15 : 24
24 Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza;

2 Wakorintho 11 : 4
4 ⑫ Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au Injili nyingine msiyoikubali, mnavumiliana naye punde!

Wagalatia 1 : 7
7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza Injili ya Kristo.

Wagalatia 2 : 4
4 Bali kwa ajili ya ndugu za uongo walioingizwa kwa siri; ambao waliingia kwa siri ili kuupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani;

Ufunuo 2 : 2
2 Ninayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wanaojiita mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;

Matendo 16 : 21
21 tena wanatangaza habari ya desturi zisizokuwa halali kwetu kuzipokea wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi.

Matendo 16 : 23
23 Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.

Matendo 18 : 13
13 wakisema Mtu huyu huwashawishi watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *