Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uzalendo
Kumbukumbu la Torati 26 : 11
11 ukayafurahie mema yote ambayo BWANA, Mungu wako, amekupa, na nyumba yako, wewe, na Mlawi, na mgeni aliye kati yako.
Zaburi 51 : 18
18 Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako, Uzijenge kuta za Yerusalemu.
Zaburi 85 : 13
13 Haki itakwenda mbele zake, Na kuzitayarishia hatua zake mapito.
Zaburi 122 : 7
7 Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
Zaburi 128 : 6
6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.
Zaburi 137 : 6
6 ⑦ Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
Isaya 62 : 1
1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
Yeremia 8 : 11
11 Kwa maana wamelitibu jeraha la binti ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.
Yeremia 8 : 22
22 ③ Je! Hakuna marhamu katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?
Yeremia 9 : 2
2 Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.
Waraka kwa Waebrania 11 : 26
26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.
Waamuzi 5 : 20
20 ⑮ Walipigana kutoka mbinguni, Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.
1 Samweli 4 : 18
18 Ikawa alipolitaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye alikuwa amewaamua Waisraeli miaka arubaini.
1 Samweli 4 : 22
22 Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa.
2 Samweli 10 : 12
12 Uwe hodari, tuwe na ujasiri, kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye BWANA afanye yaliyo mema machoni pake.
2 Samweli 11 : 11
11 Naye Uria akamwambia Daudi, Sanduku, na Israeli, na Yuda, wanakaa vibandani; na bwana wangu Yoabu, na watumishi wa bwana wangu, wamepiga kambi waziwazi uwandani; nami niende nyumbani kwangu, kula na kunywa, na kulala na mke wangu? Uishivyo, na kama roho yako iishivyo, mimi sitafanya jambo hili.
1 Wafalme 11 : 22
22 Farao akamwambia, Umekosa nini kwangu, hata, tazama, unatafuta kuirudia nchi yako? Akajibu, Hakuna, lakini unipe ruhusa tu.
Leave a Reply