Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uwajibikaji
Ezra 10 : 4
4 ⑦ Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende.
Warumi 14 : 12 – 13
12 ⑲ Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
13 Basi tusiendelee kuhukumiana, bali amueni kuwa mtu asifanye kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha.
Mathayo 6 : 9 – 13
9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Leave a Reply