Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uvumilivu
1 Mambo ya Nyakati 16 : 11
11 Mtafuteni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.
Ayubu 17 : 9
9 Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.
Zaburi 37 : 24
24 Ajapojikwaa hataanguka chini, Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
Zaburi 37 : 28
28 Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
Zaburi 73 : 24
24 Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
Zaburi 138 : 8
8 ⑯ BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.
Mithali 4 : 18
18 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.
Yeremia 32 : 40
40 ⑧ nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha, ili niwatendee mema; nami nitatia kicho changu mioyoni mwao, ili wasiniache.
Hosea 12 : 6
6 Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.
Mathayo 24 : 13
13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Mathayo 10 : 22
22 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Marko 13 : 13
13 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hadi mwisho, ndiye atakayeokoka.
Marko 4 : 8
8 Nyingine zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia.
Luka 10 : 42
42 ⑤ lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hatanyang’anywa.
Luka 22 : 32
32 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Yohana 6 : 37
37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Yohana 6 : 40
40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Yohana 8 : 32
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Yohana 10 : 29
29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
Yohana 15 : 5
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.
Yohana 15 : 7
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.
Yohana 15 : 9
9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.
Matendo 11 : 23
23 Naye, alipofika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa moyo wote.
Matendo 13 : 43
43 Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakawafuata Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.
Matendo 14 : 22
22 ⑪ wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwahimiza wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.
Warumi 2 : 7
7 wale ambao kwa subira katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoharibika, watapewa uzima wa milele;
Warumi 8 : 30
30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.
Leave a Reply