Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uvumbuzi
Mithali 8 : 12
12 Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa makao yangu; Natafuta maarifa na busara.
Mwanzo 4 : 21
21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba ya wote wapigao kinubi na filimbi.
1 Mambo ya Nyakati 23 : 5
5 na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.
2 Mambo ya Nyakati 7 : 6
6 Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao walipoagizwa; Walawi nao pamoja na vinanda vya BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.
2 Mambo ya Nyakati 29 : 26
26 ⑫ Wakasimama Walawi wenye vinanda vya Daudi, na makuhani wenye parapanda.
Amosi 6 : 5
5 ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi;
Mwanzo 4 : 22
22 Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 15
15 Huko Yerusalemu akatengeneza mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu mastadi, iwekwe juu ya minara na juu ya buruji, ili kurusha mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.
Leave a Reply