Biblia inasema nini kuhusu uvivu – Mistari yote ya Biblia kuhusu uvivu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uvivu

Mithali 24 : 30 – 34
30 Nilipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31 ⑧ Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Niliona, nikapata mafundisho.
33 ⑩ Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

2 Wathesalonike 3 : 11
11 ⑥ Maana tunasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.

2 Wathesalonike 3 : 10
10 ⑤ Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

Mhubiri 4 : 5
5 Mpumbavu huikunja mikono yake, Naye hula chakula chake mwenyewe;

1 Timotheo 5 : 13
13 Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.

Mithali 14 : 23
23 Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.

Mithali 18 : 9
9 Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharibifu.

Mhubiri 10 : 18
18 Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa ulegevu wa mikono nyumba huvuja.

Mithali 26 : 13 – 16
13 Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu.
14 Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.
15 Mtu mvivu hutia mkono wake katika sahani; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake.
16 Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu.

Mithali 23 : 21
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.

Mithali 31 : 10 – 31
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote.
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.

Mithali 21 : 25
25 Matakwa yake mtu mvivu humwua, Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.

Mithali 20 : 13
13 ⑩ Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.

Ezekieli 16 : 49
49 ⑮ Tazama, uovu wa dada yako, Sodoma, ulikuwa huu; kiburi, na kushiba chakula, na kufanikiwa, hayo yalikuwa ndani yake na binti zake; lakini hukuwasaidia maskini na wahitaji.

Mithali 6 : 6 – 11
6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7 Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu,
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9 Ewe mvivu, utalala hadi lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?
10 ① Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Mithali 10 : 26
26 Kama siki menoni, na kama moshi machoni, Ndivyo alivyo mtu mvivu kwa hao waliomwajiri.

Mithali 13 : 4
4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *