Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ushirika
Zaburi 16 : 7
7 Nitamhimidi BWANA aniongozaye, Wakati wa usiku pia moyo wangu hunishauri.
Yohana 14 : 18
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.
Yohana 14 : 23
23 ⑳ Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
1 Wakorintho 10 : 16
16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
2 Wakorintho 6 : 16
16 ⑮ Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
2 Wakorintho 13 : 14
Wagalatia 4 : 6
6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
Wafilipi 2 : 2
2 ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkiwaza mamoja.
1 Yohana 1 : 3
3 hilo tuliloliona na kulisikia, tunawahubiria na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
Mwanzo 5 : 22
22 Henoko akaenda pamoja na Mungu. Baada ya kumzaa Methusela aliishi miaka mia tatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Mwanzo 5 : 24
24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
Mwanzo 6 : 9
9 ① Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.
Mwanzo 6 : 22
22 ⑥ Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
Mwanzo 8 : 17
17 Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
Mwanzo 12 : 3
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Mwanzo 12 : 7
7 BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Mwanzo 17 : 2
2 ⑦ Nami nitafanya agano langu nawe, nami nitakuzidishia sana.
Mwanzo 18 : 33
33 Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Abrahamu, akaenda zake; Abrahamu naye akarudi mahali pake.
Mwanzo 22 : 2
2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
Mwanzo 22 : 12
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, kwa kuwa hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
Mwanzo 22 : 18
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
Mwanzo 16 : 12
12 ③ Naye atakuwa kama punda mwitu kati ya watu, mkono wake utapingana na watu wote na mkono wa kila mtu ukipingana naye; na ataishi kwa ugomvi na jamaa yake yote.
Mwanzo 26 : 1 – 360
1 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Abrahamu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.
2 BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.
3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.
4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.
5 Kwa sababu Abrahamu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
6 Isaka akakaa katika Gerari.
7 Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni dada yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.
8 Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anachezacheza na Rebeka mkewe.
9 Abimeleki akamwita Isaka, akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni dada yangu huyu? Isaka akamwambia, Kwa sababu nilisema, Nisife kwa ajili yake.
10 Abimeleki akasema, Ni nini hii uliyotutendea? Labda mtu mmojawapo angalilala na mkeo bila kufikiri, nawe ungalitutia hatiani.
11 Basi Abimeleki akawaamuru watu wote, akisema, Amgusaye mtu huyu au mkewe lazima atauawa.
12 Mwaka huo Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, naye akapata mavuno mara mia zaidi. BWANA akambariki.
13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.
14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng’ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.
15 Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Abrahamu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza udongo.
16 Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi.
17 Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko.
18 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Abrahamu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Abrahamu; naye akaviita majina kufuata majina aliyoviita babaye.
19 Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.
20 ① Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.
21 Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna.
22 ② Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
23 Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba.
24 ③ BWANA akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Abrahamu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubariki, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.
25 ④ Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA. Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko.
26 ⑤ Ndipo Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli, jemadari wa jeshi lake.
27 ⑥ Isaka akawauliza, Mbona mwanijia, nanyi mmenichukia, mkanifukuza kwenu?
28 ⑦ Wakasema, Hakika tuliona ya kwamba BWANA alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane, sisi na wewe, na kufanya mapatano nawe
29 ⑧ ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe, wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u mbarikiwa wa BWANA.
30 ⑩ Basi akawafanyia karamu, nao wakala, wakanywa.
31 ⑪ Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani.
32 Ikawa siku ileile, watumwa wa Isaka wakaja wakampasha habari za kile kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, Tumeona maji.
33 ⑫ Naye akakiita jina lake Shiba; kwa hiyo jina la mji huo ni Beer-sheba, hata leo.
34 ⑬ Esau alipokuwa mwenye miaka arubaini, akamwoa Yudithi, binti Beeri, Mhiti, na Basemathi, binti Eloni, Mhiti.
35 ⑭ Roho zao Isaka na Rebeka zikajaa uchungu kwa ajili yao.
Leave a Reply