Biblia inasema nini kuhusu Usafi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Usafi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Usafi

Kumbukumbu la Torati 23 : 14
14 kwa kuwa BWANA. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha.

Zaburi 51 : 7
7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

Zaburi 51 : 10
10 ④ Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu.

Zaburi 73 : 1
1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, Kwa hao walio safi mioyo yao.

Mithali 20 : 9
9 ⑥ Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu?

Isaya 1 : 16
16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;

Ezekieli 36 : 25
25 Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni kutoka kwa uchafu wenu wote, na kutoka kwa vinyago vyenu vyote.

1 Yohana 1 : 7
7 bali tukienenda katika nuru, kama yeye alivyo katika nuru, tunashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.

Ufunuo 1 : 5
5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *