Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia urithi
Mithali 13 : 22
22 ⑳ Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Waefeso 1 : 11 – 14
11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
12 Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.
13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, Habari Njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa mhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.
Wakolosai 3 : 23 – 24
23 Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Waefeso 1 : 18
18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
Zaburi 37 : 29
29 Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.
Mithali 20 : 21
21 ⑫ Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.
Tito 3 : 7
7 ③ ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
Matendo 20 : 32
32 Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa.
Wagalatia 5 : 19 – 21
19 ⑬ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi,
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Hesabu 27 : 6 – 11
6 BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
7 Hao binti za Selofehadi wananena lililo haki; kweli utawapa milki ya urithi pamoja na ndugu za baba yao; nawe utawapa urithi wa baba yao.
8 Kisha utanena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtu akifa, naye hana mwana wa kiume, ndipo binti yake atapewa urithi wake.
9 Tena ikiwa hana binti, mtawapa nduguze urithi wake.
10 Na ikiwa hana ndugu, mtawapa ndugu za babaye huo urithi wake.
11 Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Kumbukumbu la Torati 21 : 15 – 17
15 ⑧ Ikiwa mtu ana wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa;
16 ⑩ ndipo itakapokuwa ya kwamba siku atakayowarithisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa asiyempenda, naye ndiye mzaliwa wa kwanza huyu;
17 ⑪ lakini amkubali mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.
Luka 15 : 25 – 31
25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwa shambani na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na nderemo.
26 Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?
27 Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, akiwa mzima.
28 ⑳ Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi.
29 Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wowote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nisherehekee na rafiki zangu;
30 lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.
31 Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako.
Hesabu 36 : 6 – 9
6 BWANA ameagiza neno hili katika habari ya binti za Selofehadi, akasema, Na waolewe na waume wawapendao; lakini na waolewe katika jamaa ya kabila la baba zao.
7 ⑩ Hivyo hapana urithi wowote wa wana wa Israeli utakaotoka kabila hili kwenda kabila hili; kwa kuwa wana wa Israeli watashikamana kila mtu na urithi wa kabila la baba zake.
8 ⑪ Na kila binti atakayemiliki urithi katika kabila lolote katika wana wa Israeli, ataolewa katika jamaa moja ya kabila la baba yake, ili wana wa Israeli wapate kumiliki kila mtu urithi wa baba zake.
9 Hivyo hapatakuwa na urithi wowote utakaotoka kabila hili kwenda kabila hili; kwa kuwa makabila ya wana wa Israeli yatashikamana kila mmoja na urithi wake mwenyewe.
Warumi 8 : 17
17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Luka 12 : 13 – 21
13 Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.
14 Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?
15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
16 Akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.
Ruthu 4 : 7 – 17
7 ⑮ Basi hii ilikuwa desturi zamani za kale katika Israeli, kwa habari ya kukomboa na kubadilishana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israeli.
8 Basi yule jamaa akamwambia Boazi, Wewe ujinunulie mwenyewe. Akavua kiatu chake.
9 Naye Boazi akawaambia wale wazee na watu wote, Leo hivi ninyi ni mashahidi ya kwamba mimi nimenunua yote yaliyokuwa ya Elimeleki, na yote yaliyokuwa ya Kilioni na Maloni, mkononi mwa Naomi.
10 ⑯ Tena, huyu Ruthu Mmoabi, mkewe Maloni, nimemnunua awe mke wangu, makusudi nipate kumwinulia marehemu jina katika urithi wake, jina lake marehemu lisikatike miongoni mwa ndugu zake, wala langoni pa mji wake; leo hivi ninyi ni mashahidi.
11 ⑰ Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.
12 ⑱ Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa BWANA katika mwanamke huyu.
13 ⑲ Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na BWANA akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume.
14 ⑳ Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe BWANA, asiyekuacha leo ukiwa huna jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.
15 Naye atakurejeshea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa.
16 Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake.
17 Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi;[7] yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.
Ayubu 42 : 15
15 Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao wa kiume.
Mithali 17 : 2
2 Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.
Zaburi 16 : 6
6 Mipaka yangu imeangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri.
Leave a Reply