Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Upara
Mambo ya Walawi 13 : 41
41 Tena kwamba nywele za mtu zimemtoka kichwani upande wa mbele, yeye ni mwenye upara wa kipaji; ni safi.
Isaya 3 : 24
24 Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.
Yeremia 47 : 5
5 Upaa umeupata Gaza; Ashkeloni umenyamazishwa Mabaki ya bonde lao; Hata lini utajikatakata?
Yeremia 48 : 37
37 ⑪ Maana kila kichwa kina upara, na ndevu zote zimenyolewa; mikono yote ina alama za chale, na viuno vyote vimevikwa nguo za magunia.
Ezekieli 7 : 18
18 ⑮ Tena watajifungia nguo za magunia, na utisho utawafunika; na aibu itakuwa juu ya nyuso zote, na upaa juu ya vichwa vyao vyote.
Isaya 22 : 12
12 Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung’oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;
Yeremia 16 : 6
6 Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikatakata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;
Ezekieli 27 : 31
31 nao watajifanya kuwa na upaa kwa ajili yako, na kujifunga nguo za magunia viunoni, nao watakulilia kwa uchungu wa roho, kwa maombolezo ya uchungu.
Ezekieli 29 : 18
18 ① Mwanadamu, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alilifanyisha jeshi lake kazi ngumu juu ya Tiro; kila kichwa kilitiwa upara, na kila bega liliambuliwa ngozi, lakini hakuna mshahara uliotoka Tiro, sio wake wala wa jeshi lake, kwa kazi ile aliyofanya juu yake.
Amosi 8 : 10
10 Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upara katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.
Mika 1 : 16
16 Jinyoeni upara, jikateni nywele zenu, Kwa ajili ya watoto waliowafurahisha; Panueni upara wenu kama tai; Kwa maana wamekwenda mbali nanyi uhamishoni.
Mambo ya Walawi 21 : 5
5 ⑯ Wasijifanyie upara kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje tojo katika miili yao.
Kumbukumbu la Torati 14 : 1
1 Ninyi mmekuwa wana wa BWANA, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa.
2 Wafalme 2 : 23
23 Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!
Leave a Reply