Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uongo
Mithali 6 : 16 – 19
16 Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
17 ⑤ Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 ⑥ Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;
19 ⑦ Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
Mithali 19 : 9
9 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Naye asemaye uongo ataangamia.
Mithali 12 : 22
22 ⑤ Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.
Zaburi 101 : 7
7 Hatakaa ndani ya nyumba yangu Mtu atendaye hila. Asemaye uongo hatathibitika Mbele ya macho yangu.
Wakolosai 3 : 9 – 10
9 Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;
10 mkivaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu kulingana na mfano wake yeye aliyeuumba.
Luka 8 : 17
17 Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kuwekwa wazi.
1 Yohana 2 : 4
4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.
Waefeso 4 : 25
25 ⑫ Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.
Mithali 24 : 28
28 ⑥ Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu, Wala usidanganye kwa midomo yako.
Yohana 8 : 44
44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo.[2]
Ufunuo 21 : 8
8 ⑥ Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Mathayo 15 : 18 – 20
18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.
Kutoka 20 : 16
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
Zaburi 58 : 3
3 ③ Waovu hupotoka hata kabla ya kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.
Yakobo 3 : 14
14 ⑱ Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
Mithali 12 : 19
19 ③ Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.
Yohana 8 : 43 – 47
43 Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamuwezi kulisikia neno langu.
44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo.[2]
45 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki.
46 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?
47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 18 : 19 – 22
19 BWANA akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramoth-gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi.
20 Akatoka pepo, akasimama mbele za BWANA, akasema, Mimi nitamdanganya. BWANA akamwambia, Jinsi gani?
21 Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kufanikiwa pia; ondoka, ukafanye hivyo.
22 Basi sasa, angalia, BWANA ametia pepo wa uongo vinywani mwa manabii wako hawa; naye BWANA amenena mabaya juu yako.
Leave a Reply