Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia unyanyasaji wa kijinsia
Habakuki 1 : 3
3 Mbona wanionesha uovu, na kunifanya nione mabaya? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea.
Mwanzo 6 : 11
11 Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.
Zaburi 82 : 3
3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara;
Zaburi 72 : 4
4 Na atawatetea watu walioonewa, Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu.
Zaburi 9 : 9
9 BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida.
Mhubiri 4 : 1
1 Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Waefeso 5 : 28 – 29
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea kanisa.
Waefeso 5 : 25
25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Isaya 58 : 6
6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Isaya 10 : 1 – 2
1 Ole wao wawekao amri zisizo za haki, na waandishi waandikao sheria za kudhulumu;
2 ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake, na kuwanyang’anya maskini wa watu wangu haki yao; ili wajane wawe mateka yao, na kuwafanya yatima waliofiwa na baba zao kuwa mawindo yao!
Wagalatia 5 : 14
14 ⑩ Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Luka 4 : 18 – 19
18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
Amosi 5 : 12
12 ⑰ Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Zaburi 55 : 23
23 Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Leave a Reply