Biblia inasema nini kuhusu undugu – Mistari yote ya Biblia kuhusu undugu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia undugu

1 Yohana 4 : 20
20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.

Mithali 17 : 17
17 Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.

1 Petro 2 : 17
17 ⑮ Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

Mhubiri 4 : 10 – 12
10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kupata moto?
12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watamstahimili; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

Yohana 13 : 35
35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.

Waraka kwa Waebrania 13 : 1
1 Upendano wa ndugu na udumu.

Wafilipi 2 : 2
2 ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkiwaza mamoja.

Waefeso 4 : 29
29 ⑮ Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Yohana 13 : 34
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

Wagalatia 3 : 28
28 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.

Zaburi 133 : 1 – 3
1 Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.
2 Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
3 Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.

Malaki 2 : 10
10 Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *