Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Unafiki
Ayubu 8 : 15
15 Ataitegemea nyumba yake, isisimame; Atashikamana nayo, isidumu.
Ayubu 13 : 16
16 Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake.
Ayubu 15 : 31
31 ⑲ Asiutumainie ubatili, na kujidanganya; Kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake.
Ayubu 15 : 34
34 Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.
Ayubu 17 : 8
8 Walekevu watayastaajabia hayo, Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.
Ayubu 20 : 18
18 Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze; Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi.
Ayubu 27 : 10
10 Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi, Na kumlingana Mungu nyakati zote?
Ayubu 27 : 18
18 Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu, Na kama kibanda afanyacho mlinzi.
Ayubu 31 : 34
34 Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni.
Ayubu 34 : 30
30 Ili huyo mpotovu asitawale, Wala pasiwe na wa kuwatega watu.
Ayubu 36 : 14
14 Wao hufa wakingali vijana, Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu.
Zaburi 5 : 9
9 Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Moyo wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza.
Zaburi 50 : 17
17 Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
Zaburi 52 : 4
4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.
Zaburi 55 : 14
14 Tumehusiana vizuri; na kutembea Nyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.
Zaburi 55 : 21
21 Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
Zaburi 55 : 23
23 Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Zaburi 78 : 37
37 Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake, Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
Zaburi 101 : 7
7 Hatakaa ndani ya nyumba yangu Mtu atendaye hila. Asemaye uongo hatathibitika Mbele ya macho yangu.
Mithali 7 : 21
21 Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
Mithali 11 : 9
9 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa.
Mithali 14 : 8
8 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
Mithali 15 : 8
8 Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.
Mithali 20 : 14
14 Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu.
Mithali 21 : 27
27 Sadaka ya wasio haki ni chukizo; Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!
Mithali 23 : 8
8 Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.
Mithali 25 : 19
19 ⑰ Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.
Leave a Reply