Biblia inasema nini kuhusu Umoja – Mistari yote ya Biblia kuhusu Umoja

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Umoja

Zaburi 133 : 1
1 Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.

Isaya 52 : 8
8 Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi BWANA arejeavyo Sayuni.

Mathayo 23 : 8
8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.

Matendo 4 : 32
32 ⑬ Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walimiliki vitu vyote kwa pamoja.

Warumi 12 : 16
16 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.

Warumi 14 : 19
19 Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.

Warumi 15 : 6
6 ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

1 Wakorintho 1 : 10
10 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu migawanyiko, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.

2 Wakorintho 13 : 11
11 ⑤ Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.

Waefeso 4 : 3
3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

Wafilipi 1 : 27
27 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;

Wafilipi 2 : 2
2 ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkiwaza mamoja.

Wafilipi 3 : 17
17 Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *