Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Umaskini
Mithali 6 : 11
11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Mithali 10 : 15
15 ⑰ Mali ya tajiri ndio ngome yake; Ufukara wa maskini ndio umwangamizao.
Mithali 15 : 16
16 ① Kuwa na mali chache pamoja na kumcha BWANA; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.
Mithali 16 : 8
8 Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
Mhubiri 4 : 6
6 Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo.
Mithali 20 : 13
13 ⑩ Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.
Mithali 23 : 21
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Mithali 24 : 34
34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Mithali 28 : 19
19 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.
Leave a Reply