Biblia inasema nini kuhusu umaarufu – Mistari yote ya Biblia kuhusu umaarufu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia umaarufu

Luka 9 : 25
25 Kwa kuwa inamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akajiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?

Mithali 13 : 20
20 Nenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.

Luka 14 : 7 – 14
7 Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema,
8 Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe,
9 akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma.
10 Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe.
11 Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
12 Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika nawe ukapata malipo.
13 ① Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,
14 ② nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

Yakobo 2 : 1 – 13
1 Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu.
2 Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu;
3 nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Wewe keti hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Wewe simama pale, au keti miguuni pangu,
4 je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo maovu?
5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?
6 Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu?
7 Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?
8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.
9 Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.
10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.
12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

Mithali 29 : 25
25 ⑯ Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.

Luka 6 : 26
26 Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.

Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Mithali 3 : 1 – 4
1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.
2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
3 ① Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 ② Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

1 Petro 5 : 8
8 ⑲ Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.

2 Samweli 3 : 36
36 Wakaangalia watu wote, yakawa mema machoni pao; kama yalivyokuwa mema machoni pao yote aliyoyatenda mfalme.

Wagalatia 5 : 19 – 21
19 ⑬ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi,
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Warumi 8 : 28
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Ayubu 29 : 1 – 25
1 Kisha Ayubu akaendelea na hoja yake, na kusema,
2 Laiti ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi ya zamani, Kama katika siku hizo Mungu aliponilinda;
3 Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani, Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;
4 Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa, Hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu;
5 Wakati Mwenyezi alipokuwa angali pamoja nami, Nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka;
6 Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta!
7 Wakati nilipotoka kwenda mjini, kupitia langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,
8 Hao vijana waliniona wakanipisha, Nao wazee wakasimama kwa heshima;
9 Wakuu wakanyamaa wasinene, Na kuweka mikono yao vinywani mwao;
10 Sauti yao wakuu ilinyamaa, Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao.
11 Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia.
12 Kwa sababu nilimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
13 Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
14 ① Nilijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.
15 ② Nilikuwa macho kwa kipofu, Nilikuwa miguu kwa aliyechechemea.
16 ③ Nilikuwa baba kwa mhitaji, Na kesi ya mtu nisiyemjua niliichunguza.
17 Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake.
18 ④ Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kiota changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga;
19 ⑤ Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;
20 ⑥ Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejeshwa upya mkononi mwangu.
21 Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaza kimya wapate kusikia mashauri yangu.
22 Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu; Matamko yangu yakadondoka juu yao.
23 Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika.
24 Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha.
25 Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.

2 Samweli 15 : 2 – 6
2 ⑤ Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema, na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa, mtu yeyote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumishi wako ni mtu wa kabila fulani ya Israeli.
3 ⑥ Naye Absalomu humwambia, Tazama, maneno yako ni mema yenye haki; lakini hapana mtu aliyeagizwa na mfalme kukusikiliza.
4 ⑦ Tena Absalomu husema, Laiti mimi ningewekwa kuwa mwamuzi katika nchi hii, ili kila mtu mwenye neno au kesi aje kwangu, nimpatie haki yake!
5 ⑧ Tena ikawa hapo alipokaribia mtu yeyote kumsujudia, hunyosha mkono wake, na kumshika, na kumbusu.
6 ⑩ Hivyo ndivyo Absalomu alivyowatendea Israeli wote, waliomwendea mfalme ili wapate hukumu; na hivyo Absalomu akawadanganya watu wa Israeli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *