Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ulevi
Kumbukumbu la Torati 21 : 21
21 ⑬ Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.
Kumbukumbu la Torati 29 : 21
21 BWANA atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika kitabu hiki cha torati.
1 Samweli 1 : 14
14 Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hadi lini? Achilia mbali divai yako.
Zaburi 69 : 12
12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki.
Mithali 20 : 1
1 ③ Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.
Mithali 21 : 17
17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.
Mithali 23 : 21
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Mithali 23 : 35
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Mithali 31 : 7
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
Isaya 5 : 12
12 ⑱ Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya BWANA wala kuyafikiri matendo ya mikono yake.
Isaya 5 : 22
22 Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, na walio hodari wa kuchanganya vileo;
Isaya 19 : 14
14 Yeye BWANA ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huku na huko akitapika.
Isaya 24 : 9
9 Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; kileo kitakuwa uchungu kwao wakinywao.
Isaya 24 : 11
11 Pana kilio katika njia kuu kwa sababu ya divai; furaha yote imetiwa giza, na changamko la nchi limetoweka.
Isaya 28 : 1
1 Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!
Isaya 28 : 3
3 Taji la kiburi la walevi wa Efraimu litakanyagwa kwa miguu;
Isaya 28 : 8
8 Maana meza zote zimejaa matapiko na uchafu, hapana mahali palipo safi.
Isaya 56 : 12
12 Husema, Njooni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi.
Yeremia 25 : 27
27 Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoutuma kati yenu.
Hosea 4 : 11
11 ② Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.
Hosea 7 : 5
5 Sikukuu ya mfalme wetu, wakuu waliugua kwa ukali wa divai; alinyosha mkono wake pamoja na wenye mzaha.
Hosea 7 : 14
14 Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.
Yoeli 1 : 5
5 Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
Yoeli 3 : 3
3 ⑲ Nao wamewapigia kura watu wangu; na mvulana wamemwuza ili kupata kahaba, na msichana wamemwuza ili kupata divai, wapate kunywa.
Amosi 2 : 8
8 nao hujilaza karibu na kila madhabahu juu ya nguo zilizowekwa rehani, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya watu waliotozwa fedha.
Amosi 2 : 12
12 Lakini mliwapa Wanadhiri mvinyo wanywe; mkawaamuru manabii, mkisema, Msifanye unabii.
Amosi 6 : 1
1 Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na hao wanaokaa salama katika mlima wa Samaria, watu mashuhuri wa taifa lililo la kwanza, ambao nyumba ya Israeli huwaendea.
Amosi 6 : 6
6 ninyi mnaokunywa divai katika mabakuli, na kujipaka marhamu iliyo nzuri; lakini hawahuzuniki kwa sababu ya mateso ya Yusufu.
Leave a Reply