Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ulaji nyama
Mambo ya Walawi 26 : 29
29 ② Nanyi mtakula nyama ya miili ya watoto wenu wa kiume, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila.
Kumbukumbu la Torati 28 : 57
57 ⑧ na juu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako.
2 Wafalme 6 : 29
29 Basi, tukamtokosa mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya pili, Mtoe mtoto wako, tumle; naye amemficha mtoto wake.
Yeremia 19 : 9
9 Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.
Maombolezo 2 : 20
20 ⑩ Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?
Maombolezo 4 : 10
10 ⑭ Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.
Ezekieli 5 : 10
10 Kwa sababu hiyo baba za watu watawala wana wao kati yako, nao wana watawala baba zao; nami nitafanya hukumu ndani yako, na hao wote waliosalia kwako nitawatawanya kwa pepo zote.
Leave a Reply