Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ukombozi kutoka kwa maadui
Luka 1 : 71
71 ⑧ Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;
Wagalatia 5 : 1
1 Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Zaburi 18 : 17
17 Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
Zaburi 55 : 1 – 23
1 Ee Mungu, uisikilize sala yangu, Wala usijifiche nikuombapo rehema.
2 Unisikilize na kunijibu, Nimetangatanga nikilalama na kuugua.
3 Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi.
4 Moyo wangu unaumia ndani yangu, Na hofu za mauti zimeniangukia.
5 Hofu na tetemeko limenijia, Na hofu kubwa imeniingia.
6 Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningeruka mbali na kustarehe.
7 Ningekwenda zangu mbali, Ningetua jangwani.
8 Ningefanya haraka kuzikimbia Dhoruba na tufani.
9 Ee Bwana, uwaangamize, uzivuruge ndimi zao, Maana nimeona dhuluma na fitina katika mji.
10 Mchana na usiku huzunguka kutani mwake; Uovu na taabu zimo ndani yake;
11 Tamaa mbaya zimo ndani yake; Dhuluma na hila haziondoki mitaani mwake.
12 Kwa maana si adui aliyenitukana; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione.
13 Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.
14 Tumehusiana vizuri; na kutembea Nyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.
15 Mauti na iwapate kwa ghafla, Na washuke kuzimu wangali hai, Maana uovu uko nyumbani mwao moyoni mwao.
16 Nami nitamwita Mungu, Na BWANA ataniokoa;
17 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
18 Ameiokoa nafsi yangu iwe salama, asinikaribie mtu, Maana walioshindana nami walikuwa wengi.
19 Mungu atawalaye tangu milele atanisikia; Na kuwaadhibu, maana hawajirekebishi, Wala kumcha Mungu.
20 Mwenzangu amenyosha mkono awadhuru waliopatana naye, Amelivunja agano lake.
21 Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
22 Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
23 Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Warumi 1 : 16
16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Mgiriki pia.
Zaburi 18 : 2
2 ⑧ BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Zaburi 23 : 1 – 6
1 BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Isaya 45 : 22
22 Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.
Warumi 8 : 33
33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
Zaburi 91 : 15
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
Leave a Reply