Biblia inasema nini kuhusu Ukafiri – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ukafiri

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ukafiri

Mwanzo 3 : 1
1 ⑦ Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

Mwanzo 3 : 4
4 ⑩ Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

Kutoka 5 : 2
2 ② Farao akasema, BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui BWANA, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.

Kutoka 14 : 12
12 ⑤ Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani.

Kutoka 16 : 3
3 wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.

Kutoka 16 : 7
7 na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa BWANA; kwa kuwa yeye husikia manung’uniko yenu mliyomnung’unikia BWANA; na sisi tu nani, hata mkatunung’unikia?

Hesabu 14 : 34
34 ② Kwa jumla ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arubaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arubaini, nanyi mtakujua kuchukizwa kwangu.

Hesabu 16 : 41
41 ⑬ Lakini siku ya pili yake mkutano wote wa wana wa Israeli wakamnung’unikia Musa, na Haruni, wakasema, Ninyi mmewaua watu wa BWANA.

Hesabu 21 : 5
5 Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.

Kutoka 17 : 7
7 Akapaita mahali pale jina lake Masa,[19] na Meriba[20] kwa sababu ya ugomvi wa wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema, Je! BWANA yu kati yetu au sivyo?

Hesabu 15 : 31
31 Kwa sababu amelidharau neno la BWANA, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake.

Kumbukumbu la Torati 29 : 21
21 BWANA atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika kitabu hiki cha torati.

Kumbukumbu la Torati 32 : 15
15 Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.

1 Wafalme 20 : 28
28 Akaja yule mtu wa Mungu, akamwambia mfalme wa Israeli, akasema, BWANA asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, BWANA ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi BWANA.

1 Wafalme 22 : 24
24 ⑳ Ndipo akakaribia Sedekia, mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Roho ya BWANA alitokaje kwangu ili aseme na wewe?

2 Wafalme 2 : 24
24 Akatazama nyuma akawaona, akawalaani kwa jina la BWANA. Wakatoka dubu wawili wa kike mwituni, wakawararua vijana arubaini na wawili miongoni mwao.

2 Mambo ya Nyakati 30 : 6
6 Matarishi, kwa amri ya mfalme na maofisa wake wakapeleka nyaraka katika Israeli na Yuda yote, kusema, Enyi wana wa Israeli, mrudieni BWANA, Mungu wa Abrahamu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia ninyi mlionusurika na kuokoka toka mikononi mwa Wafalme wa Ashuru.

2 Mambo ya Nyakati 30 : 10
10 Basi matarishi wakapita mji kwa mji kati ya nchi ya Efraimu na Manase, hata kufika Zabuloni; lakini waliwacheka na kuwadhihaki.

2 Mambo ya Nyakati 32 : 19
19 ⑳ Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu, kana kwamba kuitaja miungu ya mataifa wa nchi, iliyo kazi ya mikono ya watu.

2 Mambo ya Nyakati 36 : 16
16 ⑪ lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.

Ayubu 15 : 26
26 Humshambulia na shingo ngumu, Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;

Ayubu 21 : 15
15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?

Ayubu 22 : 14
14 Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.

Ayubu 22 : 17
17 Waliomwambia Mungu, Tuondokee; Tena, Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?

Ayubu 34 : 7
7 Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu, Anywaye mzaha kama maji?

Ayubu 34 : 9
9 ⑬ Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lolote Kujifurahisha na Mungu.

Ayubu 34 : 19
19 ⑱ Sembuse yeye huwajali nyuso za wakuu, Wala hawajali matajiri kuliko maskini? Kwani wote ni kazi ya mikono yake,

Ayubu 34 : 33
33 Je! Malipo yake yatakuwa kama upendavyo wewe, hata ukayakataa? Kwani yakupasa wewe kuchagua, si mimi; Kwa sababu hiyo sema uyajuayo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *