Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ujasiri
Mithali 14 : 26
26 Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio.
Mithali 28 : 1
1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.
Waefeso 3 : 12
12 Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.
Waraka kwa Waebrania 4 : 16
16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Waraka kwa Waebrania 10 : 19
19 ⑤ Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,
Waraka kwa Waebrania 13 : 6
6 Hata tunathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
1 Yohana 2 : 28
28 ③ Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, muwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake.
1 Yohana 4 : 17
17 Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.
Mwanzo 18 : 32
32 ③ Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.
Leave a Reply