Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uhuru
Wagalatia 5 : 1
1 Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
1 Petro 2 : 16
16 ⑭ kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.
Wagalatia 5 : 13
13 ⑧ Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Yohana 8 : 32
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
2 Wakorintho 3 : 17
17 ⑮ Basi “Bwana” ndiye Roho; lakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
Warumi 8 : 1 – 4
1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
2 ⑯ Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
3 ⑰ Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
4 ⑱ ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
Isaya 61 : 1
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Warumi 6 : 18
18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.
2 Timotheo 1 : 7
7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Warumi 6 : 22
22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
Yohana 8 : 36
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
Isaya 58 : 6 – 7
6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usikose kumsaidia mtu aliye jamaa yako.
Yohana 10 : 10
10 Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu; mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.
Yakobo 1 : 25
25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Yohana 3 : 16 – 17
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Yohana 15 : 1 – 8
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi hamuwezi, msipokaa ndani yangu.
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.
6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.
8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Yeremia 33 : 3
3 ⑯ Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
1 Yohana 3 : 8
8 ⑫ atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
Kutoka 6 : 2 – 7
2 ⑭ Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni BWANA;
3 ⑮ nami nilimtokea Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi,[7] bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
4 ⑯ Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya waliyokaa kama wageni.
5 ⑰ Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.
6 ⑱ Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni BWANA nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya ukandamizaji wa Wamisri, nami nitawaokoa kutoka utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
7 ⑲ nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwakomboaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.
Leave a Reply