Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uhuishaji
Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Wakolosai 2 : 8
8 ⑩ Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
Kutoka 35 : 31 – 33
31 ⑧ naye amemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;
32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, fedha na shaba,
33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za ufundi wa kila aina.
Kumbukumbu la Torati 18 : 9 – 12
9 ⑪ Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.
10 ⑫ Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 ⑬ wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 ⑭ Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
Leave a Reply