Biblia inasema nini kuhusu ugomvi – Mistari yote ya Biblia kuhusu ugomvi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ugomvi

Waefeso 4 : 32
32 ⑱ tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Mithali 15 : 18
18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.

Mithali 15 : 1
1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.

Waefeso 4 : 29
29 ⑮ Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

1 Wakorintho 13 : 1 – 13
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wowote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;
10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.
11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga, nilifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
12 Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.
13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.

Wagalatia 5 : 19 – 21
19 ⑬ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi,
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Mithali 26 : 20
20 Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *