Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ufahamu
Zaburi 119 : 130
130 ④ Kufafanuliwa kwa maneno yako kunatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.
Mithali 14 : 29
29 Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Mithali 18 : 2
2 Mpumbavu hapendezwi na ufahamu; Ila moyo wake udhihirike tu.
Mithali 17 : 27
27 Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara.
Mithali 2 : 2 – 5
2 Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;
3 Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4 Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5 Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu.
Wakolosai 4 : 6
6 ⑥ Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
2 Timotheo 3 : 1 – 17
1 ⑧ Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 ⑩ Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
4 ⑪ wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
5 ⑫ walio na utaua kwa nje, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
6 ⑬ Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za kila namna;
7 ⑭ wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
8 ⑮ Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao wanaume wawili[1] ulivyokuwa dhahiri.
10 Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,
11 ⑯ na upendo, na subira; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
12 ⑰ Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.
13 ⑱ Lakini watu waovu na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
14 ⑲ Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao;
15 ⑳ na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Mithali 12 : 1 – 28
1 Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.
2 Mtu mwema atapata upendeleo kwa BWANA; Bali mtu wa hila atahukumiwa naye.
3 Mtu hatathibitika kwa njia ya uovu; Shina la mwenye haki halitaondolewa kamwe.
4 Mwanamke mwema ni taji la mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.
5 Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa.
6 Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.
7 Waovu huangamia, hata hawako tena; Bali nyumba ya mwenye haki itasimama.
8 Mtu atasifiwa kwa kadiri ya akili zake; Bali mwenye moyo wa ukaidi atadharauliwa.
9 Afadhali mtu anayedharauliwa, ikiwa ana mtumwa, Kuliko ajisifuye, ikiwa anahitaji chakula.
10 Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili.
11 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi hana ufahamu.
12 Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda.
13 Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu.
14 ① Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake.
15 ② Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
16 Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu.
17 Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila.
18 Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.
19 ③ Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.
20 Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.
21 ④ Mwenye haki hatapatikana na msiba wowote; Bali wasio haki watajazwa mabaya.
22 ⑤ Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.
23 Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.
24 ⑥ Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.
25 ⑦ Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neno jema huufurahisha.
26 Mwenye haki ni kiongozi wa mwenzake; Bali njia ya wasio haki huwakosesha.
27 Mtu mvivu hapiki mawindo yake; Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
28 ⑧ Katika njia ya haki kuna uhai; Wala hakuna mauti katika mapito yake.
Yakobo 1 : 2 – 4
2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Mithali 4 : 7
7 Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
Mathayo 6 : 33
33 ⑩ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Wafilipi 4 : 19
19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Mhubiri 3 : 1 – 22
1 ④ Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 ⑤ Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa kilichopandwa;
3 ⑥ Wakati wa kuua, na wakati wa kuponya; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 ⑦ Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
7 ⑧ Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
8 ⑩ Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.
9 ⑪ Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?
10 ⑫ Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.
11 ⑬ Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
12 Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi.
13 ⑭ Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.
14 ⑮ Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.
15 ⑯ Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.
16 ⑰ Zaidi ya hayo, nikaona tena chini ya jua ya kwamba, Mahali pa hukumu upo uovu, Na mahali pa haki upo udhalimu.
17 ⑱ Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi.
18 Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.
19 ⑲ Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.
20 ⑳ Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.
21 Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?
22 Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye.
Mithali 2 : 11 – 16
11 Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi.
12 Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka;
13 Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza;
14 Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotovu wa waovu;
15 Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.
16 Ili kuokoka na malaya, Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake;
Mithali 3 : 13 – 18
13 Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
14 ⑪ Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 ⑫ Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.
16 ⑬ Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
17 ⑭ Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.
18 ⑮ Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye.
Mithali 8 : 1
1 Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake?
Zaburi 34 : 13
13 ⑧ Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila.
Mithali 20 : 5
5 Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka.
Mithali 16 : 22
22 Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
Leave a Reply