Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Udi
Zaburi 45 : 8
8 Mavazi yako yote hunukia manemane Na udi na mdalasini. Katika majumba ya pembe Vinubi vimekufurahisha.
Mithali 7 : 17
17 Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini.
Wimbo ulio Bora 4 : 14
14 Nardo na zafarani, mchai na mdalasini, Na miti yote iletayo ubani, Manemane na udi, na kolezi kuu zote.
Yohana 19 : 39
39 Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta mchanganyiko wa manemane na uudi, yapata ratili mia.
Hesabu 24 : 6
6 ⑯ Mfano wa bonde zimetandwa, Mfano wa bustani kando ya mto, Mfano wa mishubiri aliyoipanda BWANA, Mfano wa mierezi kando ya maji.
Leave a Reply