Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uchumi
Mwanzo 41 : 57
57 Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote.
Mithali 24 : 27
27 Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.
Mithali 31 : 31
31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
Mhubiri 11 : 6
6 Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiulegeze mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.
Leave a Reply