Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uaminifu
Mambo ya Walawi 19 : 36
36 Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.
Kumbukumbu la Torati 16 : 20
20 Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 25 : 16
16 Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Ayubu 27 : 6
6 Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
Zaburi 7 : 4
4 ⑪ Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)
Zaburi 15 : 5
5 Asiyetoa fedha yake apate kula riba, Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.
Zaburi 24 : 4
4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiweka nafsi yake katika uongo, Wala hakuapa kwa hila.
Mithali 4 : 25
25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
Mithali 11 : 1
1 Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.
Mithali 12 : 22
22 ⑤ Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.
Mithali 16 : 11
11 ⑭ Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya BWANA; Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake.
Mithali 20 : 10
10 Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA.
Mithali 20 : 23
23 Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa BWANA; Tena mizani ya hila si njema.
Isaya 33 : 16
16 Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
Ezekieli 45 : 10
10 ⑤ Mtakuwa na mizani ya haki, na efa ya haki, na bathi ya haki.
Marko 10 : 19
19 ⑮ Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.
Luka 3 : 13
13 Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa.
Luka 6 : 31
31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.
Mathayo 7 : 12
12 ⑰ Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.
Matendo 24 : 16
16 Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.
2 Wakorintho 4 : 2
2 ⑰ lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
2 Wakorintho 7 : 2
2 ⑱ Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu yeyote, wala kumharibu mtu, wala kumkosea mtu.
2 Wakorintho 8 : 21
21 tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Wafilipi 4 : 8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Wakolosai 3 : 22
22 Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.
1 Wathesalonike 4 : 12
12 ⑱ ili mwende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu chochote.
Waraka kwa Waebrania 13 : 18
18 ⑧ Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.
1 Petro 2 : 12
12 ⑪ Muwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Leave a Reply