Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uaminifu
Zaburi 12 : 1
1 Tuokoe, ee BWANA, maana hamna tena amchaye Mungu Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.
Zaburi 31 : 23
23 Mpendeni BWANA, Ninyi nyote mlio watauwa wake. BWANA huwahifadhi waaminifu, Bali humlipiza mwenye kiburi ipasavyo.
Mithali 20 : 6
6 ⑤ Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
Mithali 28 : 20
20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Mathayo 10 : 22
22 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Mathayo 24 : 47
47 ⑬ Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
Luka 12 : 44
44 ⑭ Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
Mathayo 25 : 23
23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Luka 19 : 27
27 Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa muwachinje mbele yangu.
Luka 16 : 12
12 Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?
1 Wakorintho 4 : 2
2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.
Wagalatia 3 : 9
9 ⑤ Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Abrahamu aliyekuwa mwenye imani.
Waraka kwa Waebrania 3 : 5
5 ① Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;
2 Samweli 22 : 25
25 Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake.
1 Wafalme 19 : 10
10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.
1 Wafalme 19 : 14
14 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA, Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu waiondoe.
Leave a Reply