Biblia inasema nini kuhusu tufaha – Mistari yote ya Biblia kuhusu tufaha

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia tufaha

Wimbo ulio Bora 2 : 3
3 Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Niliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake niliyaonja kuwa matamu.

Mithali 25 : 11
11 Neno linenwalo wakati ufaao, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha.

Wimbo ulio Bora 2 : 5
5 Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.

Wimbo ulio Bora 7 : 8
8 Nilisema, Nitapanda huo mtende, Na kuyashika makuti yake. Matiti yako na yawe kama vichala vya mzabibu, Na harufu ya pumzi yako kama mapera;

Wimbo ulio Bora 8 : 5
5 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Akimtegemea mpendwa wake? Nilikuamsha chini ya huo mpera; Huko mama yako alikuonea uchungu, Aliona uchungu aliyekuzaa.

Yoeli 1 : 12
12 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imetoweka kwa wanadamu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *