Biblia inasema nini kuhusu Tobia – Mistari yote ya Biblia kuhusu Tobia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Tobia

Ezra 2 : 60
60 wazawa wa Delaya, wazawa wa Tobia na wazawa wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili.

Nehemia 7 : 62
62 Wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita na arubaini na wawili.

Nehemia 2 : 10
10 Hata Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, waliposikia habari hizi, ziliwahuzunisha sana, kwa kuwa amekuja mtu kuwatakia heri wana wa Israeli.

Nehemia 2 : 19
19 Lakini Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Ninyi mtaasi juu ya mfalme?

Nehemia 4 : 3
3 Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.

Nehemia 4 : 8
8 wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo.

Nehemia 6 : 14
14 ⑧ Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati kulingana na hayo matendo yao, na yule nabii mwanamke Noadia.[7]

Nehemia 6 : 19
19 Tena waliyanena mema yake mbele yangu, na kumwambia maneno yangu. Tobia naye akaniletea mimi nyaraka za kuniogofya.

Nehemia 6 : 18
18 Kwa maana walikuwa watu wengi katika Yuda waliomwapia, kwa sababu alikuwa mkwewe Shekania, mwana wa Ara; naye Yehohanani mwanawe amemwoa binti Meshulamu, mwana wa Berekia.

Nehemia 13 : 9
9 Kisha nikatoa amri, nao wakavisafisha vyumba; nami nikavirudisha humo vyombo vya nyumba ya Mungu, pamoja na sadaka za unga na ubani.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *