Biblia inasema nini kuhusu Terafi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Terafi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Terafi

Mwanzo 31 : 19
19 Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye.

Mwanzo 31 : 35
35 Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.

Waamuzi 17 : 5
5 Basi mtu huyo Mika alikuwa na nyumba ya miungu, naye akafanya naivera, na kinyago, akamweka wakfu mmoja miongoni mwa wanawe, akawa kuhani wake.

Waamuzi 18 : 14
14 Ndipo hao watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laisha wakawaambia ndugu zao, Je! Ninyi mwajua ya kwamba mna naivera ndani ya nyumba hizi, na kinyago na sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu? Basi sasa fikirini iwapasayo kufanya.

Waamuzi 18 : 20
20 Huyo kuhani moyo wake ukafurahi, naye akaitwaa hiyo naivera, na kile kinyago, na hiyo sanamu ya kuchonga, akaenda katikati ya hao watu.

Mwanzo 35 : 4
4 ⑥ Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na vipuli vilivyokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *