Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Tekoa
2 Mambo ya Nyakati 11 : 6
6 Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa,
2 Samweli 14 : 2
2 Yoabu akatuma watu waende Tekoa, akaleta kutoka huko mwanamke mwenye akili, akamwambia, Nakusihi, ujifanye kama unaomboleza, ukavae nguo za kufiwa, nakusihi, wala usijitie mafuta, ila ukafanane na mwanamke aliyeomboleza siku nyingi kwa ajili yake aliyefariki;
2 Samweli 14 : 4
4 Naye yule mwanamke wa Tekoa aliponena na mfalme, akaanguka kifudifudi chini, akamsujudia, akasema, Nisaidie, Ee mfalme.
2 Samweli 14 : 9
9 Ndipo huyo mwanamke wa Tekoa akamwambia mfalme, Na uwe juu yangu, Ee bwana wangu mfalme, na juu ya nyumba ya baba yangu uovu huu; wala kwa mfalme na kwa kiti chake cha enzi pasiwepo hatia.
2 Mambo ya Nyakati 11 : 6
6 Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa,
2 Mambo ya Nyakati 20 : 20
20 ③ Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.
Nehemia 3 : 5
5 ① Na baada yao wakajenga Watekoi; lakini wakuu wao hawakutia shingo zao kazini mwa bwana wao.
Nehemia 3 : 27
27 Baada yake wakajenga Watekoi sehemu nyingine, kuuelekea mnara mkubwa utokezao, na mpaka ukuta wa Ofeli.
Yeremia 6 : 1
1 Kimbieni mpate kuwa salama, enyi wana wa Benyamini; tokeni katika Yerusalemu, pigeni tarumbeta katika Tekoa, simamisheni ishara juu ya Beth-hakeremu; kwa maana mabaya yanachungulia toka kaskazini, na uharibifu mkuu.
Leave a Reply