Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Spikenard
Wimbo ulio Bora 4 : 14
14 Nardo na zafarani, mchai na mdalasini, Na miti yote iletayo ubani, Manemane na udi, na kolezi kuu zote.
Wimbo ulio Bora 1 : 12
12 Muda mfalme alipoketi juu ya kochi, Nardo yangu ilitoa harufu yake.
Marko 14 : 3
3 Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mwenye ukoma, akiwa amekaa mezani, alikuja mwanamke mwenye chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa; akaivunja chupa akaimimina kichwani pake.
Yohana 12 : 3
3 Basi Mariamu akatwaa ratili ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.
Leave a Reply