Biblia inasema nini kuhusu Sodoma – Mistari yote ya Biblia kuhusu Sodoma

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sodoma

Mwanzo 19 : 8
8 Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mwanamume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.

Kutoka 22 : 19
19 Mtu yeyote alalaye na mnyama sharti atauawa.

Mambo ya Walawi 18 : 23
23 ⑥ Wala usilale na mnyama yeyote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni upotovu.

Mambo ya Walawi 20 : 13
13 ① Tena mwanamume akilala pamoja na mwanamume, kama alalavyo na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.

Mambo ya Walawi 20 : 16
16 Tena mwanamke akimmwendea mnyama yeyote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao.

Kumbukumbu la Torati 23 : 17
17 Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.

Kumbukumbu la Torati 27 : 21
21 ⑭ Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yoyote. Na watu wote waseme, Amina.

Waamuzi 19 : 22
22 ⑬ Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu mabaradhuli wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani kwako, ili tupate kumjua.

1 Wafalme 14 : 24
24 Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.

1 Wafalme 15 : 12
12 ⑪ Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake.

1 Wafalme 22 : 46
46 Tena mahanithi waliosalia, hao waliosalia siku za Asa baba yake, akawaondoa katika nchi.

2 Wafalme 23 : 7
7 ⑫ Akaziangusha nyumba za mahanithi, waliokuwamo nyumbani mwa BWANA, wanawake walipofuma mapazia ya Ashera.

Warumi 1 : 24
24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.

Warumi 1 : 27
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

1 Wakorintho 6 : 9
9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *