Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sifa
Kutoka 15 : 19
19 Kwa maana farasi wa Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.
Kutoka 15 : 21
21 Miriamu akawaitikia, Mwimbieni BWANA kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
1 Samweli 2 : 10
10 ① Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi[2] wake.
1 Mambo ya Nyakati 16 : 36
36 Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA.
1 Mambo ya Nyakati 29 : 19
19 naye Sulemani mwanangu, umjalie ili kwa moyo wote, azishike amri zako, na shuhuda zako, na maagizo yako, akayatende hayo yote na kuijenga nyumba hii ya enzi, niliyoiwekea akiba.
2 Mambo ya Nyakati 5 : 13
13 hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA,
Zaburi 46 : 11
11 BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio[8] letu.
Zaburi 48 : 14
14 Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.
Zaburi 76 : 12
12 ⑬ Yeye huzikata roho za wakuu; Na kuwatisha wafalme wa dunia.
Zaburi 85 : 13
13 Haki itakwenda mbele zake, Na kuzitayarishia hatua zake mapito.
Zaburi 98 : 9
9 Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja kuihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu, Na mataifa kwa adili.
Leave a Reply