Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shukrani
Mathayo 11 : 25
25 Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Mathayo 26 : 27
27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Kuyweni nyote katika hiki;
Yohana 11 : 41
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
Ufunuo 4 : 9
9 Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,
Ufunuo 7 : 12
12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.
Ufunuo 11 : 17
17 wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki.
Zaburi 50 : 14
14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.
Zaburi 50 : 14
14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.
1 Timotheo 1 : 12
12 Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;
Warumi 1 : 8
8 Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubiriwa kote duniani.
Wakolosai 3 : 17
17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.
Waraka kwa Waebrania 13 : 15
15 ⑤ Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake.
Waefeso 5 : 20
20 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
2 Wakorintho 1 : 11
11 ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba, ili, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu.
Danieli 6 : 10
10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kuelekea Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Zaburi 35 : 18
18 Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi.
1 Wathesalonike 5 : 18
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Leave a Reply