Biblia inasema nini kuhusu Shilo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Shilo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shilo

Mwanzo 49 : 10
10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.

Waamuzi 21 : 19
19 Kisha wakasema, Angalieni, iko sikukuu ya BWANA mwaka baada ya mwaka katika Shilo, mji ulio upande wa kaskazini mwa Betheli, upande wa mashariki mwa hiyo njia kuu iendeayo kutoka Betheli kwenda Shekemu, nao ni upande wa kusini mwa Lebona.

Yoshua 18 : 1
1 Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao.

Yoshua 18 : 10
10 Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.

Waamuzi 18 : 31
31 ① Basi wakaiabudu hiyo sanamu ya kuchonga aliyotengeneza Mika, wakati wote ile nyumba ya Mungu ilipokuwako huko Shilo.

Waamuzi 21 : 19
19 Kisha wakasema, Angalieni, iko sikukuu ya BWANA mwaka baada ya mwaka katika Shilo, mji ulio upande wa kaskazini mwa Betheli, upande wa mashariki mwa hiyo njia kuu iendeayo kutoka Betheli kwenda Shekemu, nao ni upande wa kusini mwa Lebona.

1 Samweli 1 : 3
3 Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.

1 Samweli 1 : 9
9 Ndipo Hana akainuka, walipokula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la BWANA.

1 Samweli 1 : 21
21 Kisha yule mtu, Elkana, na watu wote wa nyumbani mwake, wakakwea kwenda kumtolea BWANA dhabihu ya mwaka, na nadhiri yake.

1 Samweli 1 : 24
24 Naye alipomwachisha kunyonya, akamchukua pamoja naye, na ng’ombe watatu,[1] na efa moja ya unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa BWANA, huko Shilo; na yule mtoto alikuwa mtoto mdogo.

1 Samweli 2 : 14
14 naye huutia kwa nguvu humo chunguni, au birikani, au sufuriani, au chomboni; nyama yote iliyoinuliwa kwa huo uma kuhani huichukua mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokuja huko.

Zaburi 78 : 60
60 ⑯ Akaiacha maskani ya Shilo, Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu;

Yeremia 7 : 12
12 ⑰ Lakini nendeni sasa hadi mahali pangu palipokuwapo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone nilivyopatenda kwa sababu ya uovu wa watu wangu Israeli.

Yoshua 21 : 2
2 wakanena nao hapo Shilo katika nchi ya Kanaani, wakisema, Yeye BWANA aliamuru kwa mkono wa Musa kwamba sisi tupewe miji tupate kukaa humo, mbuga zake za malisho kwa ajili ya mifugo wetu.

Yoshua 22 : 9
9 ⑯ Basi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase wakarudi, wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.

Yoshua 22 : 12
12 ⑱ Basi, wana wa Israeli waliposikia habari hiyo, mkutano wote wa wana wa Israeli wakakutanika pamoja huko Shilo, ili waende kupigana nao.

Waamuzi 21 : 12
12 ⑤ Nao wakapata katika wenyeji wa Yabesh-gileadi wanawali mia nne, ambao hawajamjua mwanamume kwa kulala naye; basi wakawaleta kambini huko Shilo, ulioko katika nchi ya Kanaani.

1 Samweli 1 : 9
9 Ndipo Hana akainuka, walipokula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la BWANA.

1 Samweli 4 : 13
13 Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *